Lyrks
Lyrks
Lyrks
Cover Art

Elimu Dunia Lyrics by Daz Baba

Elimu Dunia

2004

[Verse 1: Daz Baba]
Fikra za ajabu, kiburi pamoja na zogo
Nilionekana nnazo tangu nikiwa mdogo
Michezo ya hatari pamoja na dhuluma
Kiburi kwa wakubwa zangu walipo nituma
Ndipo wazazi wangu walikaa chini wakafikiri
Japokuwa mimi mkubwa nianze skuli
Ndipo nlipoanza la kwanza mpaka la pili
Ambapo kamari na jeuri vikawa vimeshamiri
Nikasogea sogea mpaka darasa la tatu
Hapo nikazidi kuikata elimu katu katu
Maombi ya wazazi na mswalia mswalia mtume 'ndivyo vilivyo nisaidia mi kufika la nne
Ambapo nkakataa shule ’nikawa nipo zangu tu maskani
Huku nikitathmini mali za majirani
Leo nikavunje pale 'kwa tajiri flani
Ili mradi tu nipate chochote kile kinywani
Hakika nilifanya kila aina ya unyama
Ofisi yangu ufunguliwa jua lilipo zama
Nnacho kumbuka mama yangu alilia sana
Hata baba katishia kuniachia laana
[Chorus: Daz Baba]
Elimu Dunia 'mwenzenu nilikataa
Elimu Dunia ’mwenzenu nilikataa
Nilipenda maasi nimekumbwa na balaa
Maisha yangu yote naishia mfungwa
Elimu Dunia 'mwenzenu nilikataa
Mwenzenu nilikataa
Nilipenda maasi nimekumbwa na balaa
Maisha yangu yote naishia mfungwa
Elimu Dunia
[Verse 2: Daz Baba]
Washkaji walikuwa wakija nigongea night kali
"Kamanda, amka! twende tukausake utajiri"
Hata kwa njia zile ambazo sio halali 'nikakubali, nikawa silali
Nafanya vile akili yangu ilivyo nituma Navunja mlango hata kwa jiwe fatuma
Yeyote aliye leta ubishi kutoa mali 'alitolewa uhai
Nlichokuwa nkitaka kwake 'kwanza ni maslahi
Maasi yangu mwisho yakaongezeka
Habari kwenye vyombo vya dola kote zikafika
Matangazo kwenye magazeti sasa kaandikwa
Jambazi muhalifu 'anatafutwa
Na donge nono itatolewa endapo atakamatwa
Huwezi kuamini kweli arobaini zake mwizi
Siku hiyo kwenye kazi 'nimenasa kitanzi...
Naishia gerezani
[Chorus]
Elimu Dunia 'mwenzenu nilikataa
Elimu Dunia ’mwenzenu nilikataa
Nilipenda maasi nimekumbwa na balaa
Maisha yangu yote naishia mfungwa
Elimu Dunia ’mwenzenu nilikataa
Mwenzenu nilikataa
Nilipenda maasi nimekumbwa na balaa
Maisha yangu yote naishia mfungwa
Elimu Dunia
[Verse 3: Afande Sele]
We ni mfungwa sasa 'si mtu huru
Ukilalamika sana utakuwa kama unakufuru tu
Lazima ujue sisi ni vifaranga na maisha ni kama mwewe
Mama yetu ni elimu’ ulio mkataaga we mwenyewe zamani
Ulimkataa elimu ya duniani 'ukampiga hadi mwalimu darasani
Hukusikia la (?) wala la (?) Swala hukuliamini
Umri ulikudanganya ukawa mbabe shuleni
Sasa ndio hivyo uko nasi gerezani
Jiamini mdogo wangu 'kwani jela sio kaburini au kwa Mungu
Umetengwa na jamii, hujatengwa na dunia hii
Jifunze kupokea furaha sawa na huzuni
Kumbuka kwamba tabu na raha zipo duniani
Zipo kwa ajili ya watu na watu ndio mi na wewe
Kila mmoja atabeba madhambi yake mwenyewe 'imeandikwa
Kama umekunywa sumu sasa ya nini uombewe? Eenh?
Sasa ya nini uombewe?
Yeah
[Verse 4: Ferooz]
Yeah, yeah, yeah, yeah, yeah, yooh
Anhaa, yeah, yooh
Nimewaharibia hadi ndugu na jamaa Nimekosa hata wakuniekea dhamana
Ndege mjanja asiye naswa nimeishia ukingoni
Mabawa yamekatika mwokozi mi simuoni
Uraiani kurudi ’sidhani...
Daz Nundaz, Scout Jentaz, Sewa Side
Tamaa zilinifanya niwe gaidi
Fikra zangu ulimwengu nitaumudu
Leo una nifunza kwa mola na tubu
Yah maulana niokoe 'kwenye gharika mcha wako nitoe
Leo ndio usemi umetimia
Hauna kilio msiba wakujitakia
[Chorus]
Elimu Dunia 'mwenzenu nilikataa
Elimu Dunia 'mwenzenu nilikataa
Nilipenda maasi nimekumbwa na balaa
Maisha yangu yote naishia mfungwa
Elimu Dunia 'mwenzenu nilikataa
Mwenzenu nilikataa
Nilipenda maasi nimekumbwa na balaa
Maisha yangu yote naishia mfungwa
Elimu Dunia
[Instrumentals]
Credits

About “Elimu Dunia” by Daz Baba

Read the complete lyrics to "Elimu Dunia" by Daz Baba from the album "Elimu Dunia" in 2004. On Lyrks you can follow along with the full text, explore the artist's discography, and discover related songs. The track is often categorized under Bongo Flava, Rap, Tanzania.

"Elimu Dunia" is performed by Daz Baba. from the album "Elimu Dunia" in 2004 This page provides the full lyric text for fans who want to sing along, study the songwriting, or compare versions across releases. Lyrks organizes lyrics by artist and song slug so you can bookmark and share a stable URL. Music lyrics help listeners connect with emotion, narrative, and rhythm in a track. Whether you are learning English, researching a favorite chorus, or preparing for karaoke, having accurate line breaks and section labels (verse, chorus, bridge) makes the experience easier. We link to the official artist profile on Lyrks where available, including biography snippets, top songs, and chart placements when we have that data. If you enjoy "Elimu Dunia", explore more songs by Daz Baba using the links below. Chart and trending pages on Lyrks highlight what listeners are searching for this week. For copyright or correction requests, see our DMCA and contact pages.

View all songs and biography for Daz Baba · Trending lyrics · Billboard Hot 100

Frequently asked questions

"Elimu Dunia" is credited to Daz Baba. Songwriting credits may include additional writers listed on the release; check the credits section on this page for linked collaborators.

"Elimu Dunia" appears on "Elimu Dunia" in 2004.

Visit the Daz Baba artist page at /artist/daz-baba for biography, popular tracks, and links to more lyric pages.