Lyrks
Lyrks
Sign In
Cover Art

Starehe Lyrics by Ferooz

Safari

0

[Chorus: Ferooz]
Hapa nilipo mimi nipo kitandani
Starehe zimeniweka matatani, kupona tena haiwezekani
Masela wangu, ndugu zangu buriani
Kwaherini
Kwaherini
Kwaherini
Sewa Side, Scout Jentaz 'kwaherini
Bongo Records na Majani 'kwaherini
Hamtoniona tena duniani
Sasa najuta, mwenzenu yamenikuta
Ibilisi amefanikiwa kunivuta
Sasa sijui wakumlaumu nani 'kati ya nafsi yangu ama shetani
Kwaherini
Kwaherini
Kwaherini
Makongo na Jite Ute, kwaherini
(?) na Azania, kwaherini
Ah aah aaah...

[Verse 1: Ferooz]
Ni saa saba juu ya alama saa nikiitazama
Nimesha achana na Jackie sasa namfuata Salama
Saa kumi na mbili na appointment na mademu wawili 'achana na Lily ambaye tutakutana saa mbili
Jane wa Mikocheni ambaye sasa hayupo duniani aliye kuwa akinisubiri pale Vaticani kijiweni
Minah na Semeni tunakutana kwa Macheni
Na kila siku niliwabadilisha tena kwa foleni
Huo ndio ulikuwa mwenendo wa maisha yangu, mimi viwanja kujivinjari na machangu...
Oooh, niliona fahari... yeah
Starehe mi nilizifanyia papara, nilibadili mademu kama vidaladala
Nikienda nimepanda hili, nikirudi lile 'nilitamani starehe zote nizitawale
Hata kumkumbuka mola wangu ilikuwa ndoto
Nilitekwa na ulimwengu kumbe na ukimbilia moto
Tabia za kubadili wasichana nilikubuhu
Nilitembea na watoto wa geti, machangu na ma-sista doo
Ubaya kwamba Condom sikuitambua
Kwa kujua kwamba ladha ya mapenzi itapungua
Kumbe nilikuwa ninapotea njia 'nlioshauriwa mimi nikapuuzia
Idadi ya wanawake ikawa lukuki, ikapita kipindi wengine nikawa siwakumbuki
Ona, ona...
Ona sasa yaliyo nisibu kwa dada yake Bashiri
Nilishamsahau kama tulishakutana kimwili nilivyo muona nikamtongoza tena, tena kwa mara ya pili
Ona sasa, ah aah aaah

[Chorus: Ferooz]
Hapa nilipo mimi nipo kitandani
Starehe zimeniweka matatani, kupona tena haiwezekani
Masela zangu, ndugu zangu buriani
Kwaherini
Kwaherini
Kwaherini
Afande Sele 'Morogoro, kwaherini
Arusha, wanapolo, kwaherini
Hamtoniona tena duniani
Sasa najuta, mwenzenu yamenikuta
Ibilisi amefanikiwa kunivuta
Sasa sijui wakumlaumu nani 'kati ya nafsi yangu ama shetani
Kwaherini
Kwaherini
Kwaherini
Discipline Camp na Wa Kush, kwaherini
Sinza Star na Choka Mbaya, kwaherini
Ah aah aaah

[Verse 2: Prof. Jay & Ferooz]
Kijana vipi?
Mbona hujagonga mlango?
Jipange kwenye foleni, mmoja mmoja ndio mpango
Ondoa mashaka tiba bora haitaji haraka
Subiri watibiwe wenzako nawe utafata
Dokta, mimi nimekuja kufanya hitimisho, naamini hii ndio itakuwa ungwe yangubya mwisho
Dalili zinaonesha nimeathirika na nimekuja pima tu nipate uhakika
Ebu cheki dokta nilivyo konda, nimebakia mifupa, mwili umetapakaa vidonda
Vipele usiseme hii yote dalili ya umeme, dalili ya umeme...
No! Acha uoga hata Malaria iko namna hii
Unaweza ukakonda kwa Typhoid au T.B
Ukinificha una hatarisha maisha, ni bora kubainisha kipi kinakutisha, eh?
Homa za mara kwa mara kwangu hazikatiki, kuharisha mara sitini na mbili kwa wiki
Eenh angalia hata nywele zilivyo nyonyoka, mabega yamepanda juu utasema yanachomoka
Ninao, ninao
Supiri vipimo!
Ninao, ninao
Usikate tamaa!
Ninao, ninao
Dokta usinipe moyo, ni sawa unampa mfupa autafune kibogoyo
Duniani mimi sina umuhimu, kuiaga dunia inapaswa, ina nilazimu
Ni bora nijue tu, nielekee kuzimu
No!, no!, hayo ni maamuzi ya ajabu, na ni ulimbukeni kujiua pasipo sababu
Maradhi ni kawaida kwa binadamu hilo fahamu
Ni vyema ungetulia upate majibu ya damu
Sasa kumbe wewe unaona mimi nasubiri nini, ni bora tu niwahi kupumzika kaburini
Starehe mnazipenda ila mwisho wake mbaya, wengi wameteketea kwa kuendekeza umalaya
Vipimo vinaonesha ni kweli umeathirika, I'm very sorry, kupoteza nguvu ya taifa
Ni vyema kufanya ibada na kumrudia muumba wako, kula vizuri, fanya mazoezi, pumzisha mwili wako
Ukizingatia hayo utaishi kwa matumaini
By the way, unayo nafasi hebu jiamini
Mola aliye niumba sasa nishamkosea, ( Pole kijana )
Hata ardhi na mbingu zote zinanizomea, malaika wa zamu kwa hamu wananingojea
Nikifika huko nani atanipokea...?
Ah aah aaah

[Chorus: Ferooz]
Hapa nilipo mimi nipo kitandani
Starehe zimeniweka matatani, kupona tena haiwezekani
Masela wangu, ndugu zangu buriani
Kwaherini
Kwaherini
Kwaherini
Wa bara na visiwani, kwaherini
T.M.K., Kino Plane, kwaherini
Hamtoniona tena duniani
Sasa najuta, mwenzenu yamenikuta
Ibilisi amefanikiwa kunivuta
Sasa sijui wakumlaumu nani 'kati ya nafsi yangu ama shetani
Kwaherini
Kwaherini
Kwaherini
Kikosi cha mizinga, kwaherini
Migo migo Sinza, kwaherini
Ah aah aah
Ah, ah

( Instrumentals )
Credits

About “Starehe” by Ferooz

Read the complete lyrics to "Starehe" by Ferooz from the album "Safari". On Lyrks you can follow along with the full text, explore the artist's discography, and discover related songs. The track is often categorized under R&B.

"Starehe" is performed by Ferooz. from the album "Safari" This page provides the full lyric text for fans who want to sing along, study the songwriting, or compare versions across releases. Lyrks organizes lyrics by artist and song slug so you can bookmark and share a stable URL. Music lyrics help listeners connect with emotion, narrative, and rhythm in a track. Whether you are learning English, researching a favorite chorus, or preparing for karaoke, having accurate line breaks and section labels (verse, chorus, bridge) makes the experience easier. We link to the official artist profile on Lyrks where available, including biography snippets, top songs, and chart placements when we have that data. If you enjoy "Starehe", explore more songs by Ferooz using the links below. Chart and trending pages on Lyrks highlight what listeners are searching for this week. For copyright or correction requests, see our DMCA and contact pages.

View all songs and biography for Ferooz · Trending lyrics · Billboard Hot 100

Frequently asked questions

"Starehe" is credited to Ferooz. Songwriting credits may include additional writers listed on the release; check the credits section on this page for linked collaborators.

"Starehe" appears on "Safari".

Visit the Ferooz artist page at /artist/ferooz for biography, popular tracks, and links to more lyric pages.


Lyrks
Lyrks

Your gateway to the world of music lyrics.

Product

Features


© 2026 Lyrks. All rights reserved.