SLEEPING PILLS
Baby, niko na five loaves za words for you, ju uko morally starving
Honey, niko na two fish za stinking metaphors for you too, ju uko eternally deserving
Nipe a piece of your vestibule ama nita-claim sikio moja lako likiwa full ka the biblical Peter
Ukini-deter, hautaki niiseme out loud, then I beg to differ
Naeza kasirika niku-strangle so please keep your distance
Sikujua that you’re such a stinking frenemy
Ulinifanya niamini hip hop is all about hatred na ma-fellow MCs ni ma-enemy
Sitatumia marungu na mapanga kukuonyesha vile wewe ni vidole za shetani
Nitatumia the samе hip hop, call it re-inventing the languagе of the enemy
Bado nakumbuka vile tulipatana
Memories na picha ni clear kwa akili ni kama
Nilijua na smile ya virgin, tuki-flirt baada yetu kukutana jana
Kwa radio na TV ulikuwa in
Kwa gazeti, internet, pia kwa magazine
Kwa posters, banners, na kwa adverts za condom na margarine
Si ni figure yako na colour ya skin ziliacha macho na marbles kwa skull ziki-spin
I mean, ma-boy kukufurahisha, walitoboa masikio na wakaekelea tattoo kwa skin
Nili-contemplate lakini wazazi waka-intervene
Kwani kwa battle between mi na wewe, ulikuwa una-appear ku-win
Nilijaza picha zako kwa dawati niki-imagine mimi na wewe
Kitu ilinifanya darasani anything nisielewe
Nili-share story zako na ma-agemate wakaniambia si possible mi kuwa na wewe
Kwani place ulipatikana ni kwa vilabu ka F2, niliku-pay visit
Waliona ni mapema kwangu ku-join dunia illicit
Kwa kila kitu ulifanya ilikuja na warning za “parental advisory” kama content explicit
Kwa kioo, nilijiandaa vile ningekuwa noticed na wewe
Si craving ilikuwa hyper
Hardwork pays, nilikuandikia mashairi na barua kila ngware nikirauka
Kwa corner za mitaa na hood, sessions za beat box, nilikutaja kwa cypher
Apart from wasichana wali-wave na ma-boy walinitambua kwa mitaa, watu wachache bado walinipatia wiper
Attention nilipata haikuwa enough, I had to grow wiser
Target yangu na matarajio ilikuwa nijulikane even beyond taifa
Finally, ulintokea na glory ya bikra amevaa buibui
Mi kugundua ulikuwa Cleopatra, stupid, ilikuwa ngumu
Cupid na arrows za sumu
Baadaye ulinipa roho yako, nilijisikia winner
Ever since kuitana majina ka “honey”, “sweety” na “baby” kwa meza za dinner
Kuku-keep, nywele nikafuga, maskio nikazidunga stud ka Willy Mutunga
Kwa speech, cursing words nikazikuza
Nikaanza kumeza steroids na kuinua weight enough ndio kuunga
Kumaliza stage fright, ukanifunza ku-puff puff na ku-sniff unga
Bado nilikuwa na crisis moja
Ngoma zangu hazikuchezwa kwa radio
Reason ulinipa ni ati maskio za ma-fans huwa kwa makalio
Jina na flow nikabadilisha
Topics nika-change, nikaanza kuwaambia, “Ass tingisha! Glass gonganisha!”
Badala ya kuongelea issues zingeacha plus kwa hii maisha
For a moment nilikuwa kwa vita na conscience yangu
Ju truth from the beginning ilikuwa ni creed
Conscience ikakuwa ina-bleed, erection ika-take the lead
Utakuzaje morals kwa kichwa imejaa weed?
Record deal, nililetewa more than enough
Lust ya fame ikageuza roho yangu ikakuwa rough
Printing press zilijaza my photographs
Nili-get millions tokana na merchandise na phonographs
Desperate women walinitolea boobs for autographs
Media zilini-quote like never before, ju siku-wean words from chaff
Superstar kwa discography
Hormones za fame zilinikimbia, ukani-lure into pornography
Coz of you nika-sell out truth, essence, poetry na soul philosophy
For awards, deals, media coverage na trophies
Trophies filled up with nothingness to the brim zilifanya ma-youth kuni-copy
Waliniona ma-role model, BBC wakakuza my biography
Ma-manager, ma-presenter na ma-promoter, waliokota shilingi zao through mikono yangu
Media walipenda ngoma zangu wakati nilisifu vanity kwa mistari zangu
Ukani-introduce kwa kingdom ya darkness, ukani-convince niuze soul yangu
Ndio nipate a lot of followers kwa social network na website yangu
Niliishi siku mbili kwa moja ni ka dunia yote ilikuwa yangu
Twerks zako zikani-introduce kwa Western culture, nikapuuza morals zangu
Nikasahau life is returnable gift
Sahii between me na God kuna a very big rift
Heavens ziko so many miles away, akili poisoned by the rot ya addiction
Kila kitu inani-trick
Najaribu kujitoa, spirit ni willing but mwili ni weak
I miss hip hop, I miss the snare, I miss the kick
I miss healing, if only God could speak
Coz all I know nikuimbia tits, kusifu pesa, pombe, magari na freaks
It’s irrelevant kila song natoa ni hit
Dear music industry, wewe ni bitch
And I’m sure huwezi kana
Nilikupenda sana, sahii guilt na majuto zinaniandama
Ulini-promise an eternal knight in shining armour
How comes mi ni loser in aluminium foil plus napigana na karma?
Demands zako ni reason kuna too many funerals za ma-emcee
Too many ephemera career za ma-emcee
Una-disrespect wanawake reason kuna less female emcees
Umegeuza wengi real wakuwe players shinda media za VLC
For now I’m leaving, God bless all the hip hop emcees
Elvis Presley, Amy Winehouse, Tupac, Biggie, Whitney, MJ
Najua pride nikiwataja is what u-feel
I’m off kuwa-join, after nime-swallow hii overdose ya sleeping pills