Lyrks
Lyrks
Lyrks
Cover Art

Fungua Lyrics by Rapcha

To The Top Vol.2

2023

Oya mwanangu vipi?
99 mwanangu
Mbona kinyonge?
Ahhh hamna ishu wala nini
Ndo shida hiyo ya kubetia team msizozijua hahah
Ahh sio kubet
Najua babu
Ila umekaa kimya kinoma nini shida mwanangu ni kweli..!!
We acha tu mwanangu si unamuelewa huyu shemeji yako jinsi ambavyo nna mkubali
Aah naelewa
Halafu kuna miyeyusho flani anakua ananiletea ambayo sio
Yani kama hivi kuna story ambazo mi nakua nazisikia halafu nikitaka kumwambia yani koo langu linakua kama kuna kitu kimenishikilia hapa nashindwa kuongea yani
Kwasababu najua nikimgusa tu hivi kidogo anakasirika anakuja juu ila nataka kinoma kumchana sa sjui tu naanzia wapi mwanangu
Aaah Kwahiyo tatizo ndio hilo?
Ndio hivyo mwanangu
Chukua kwanza kitu hichi
Au sio
Piga mbili ukimaliza hicho mwanangu utakua na nguvu ya kumchana mbona suala dogo
Kula kitu maliza mchane
Uhakika??
Imeisha hiyo baba
Mmmh naam naam
Uuuu chapa chapa chapa yeah yeah ye ye yeee
Mambo mengine mambo madogo mwanangu anakua anawaza
Cough!! Mwanangu hiki kama chenye
Msumbiji hiyo baba
Sasa mwanangu
Oi oi oi
Hebu Ngoja mi nicheze (mara moja hii umemaliza kitu??)
Ngoja Nimkute huko huko aliko nikamuanzishie kama vipi
Aina noma simu zilie mzee simu zilie babaaa
Door bell rings
Hizi kengele huyu anahisi nacheza nini?
Fungua inamaana huskii hii kengеle au utaka nije tu kukulabua
Kama mnafichana ndani ya makabati leo nitawasha moto hii nyumba ndo mtanitambua
Skia еm fungua usitake nijaze watu waje waokote tu vipande maana watakuta nishakupasua
Sasa basi napiga kengele mara ya mwisho na navunja kama hutaki kufungua
Oya em Fungua ushaniweka zaidi ya nusu saa nakubishia hodi hutaki kufungua
Ila Hawa kenge wanaokufata sehemu nayolipa kodi wakigonga mlango na miguu unafungua
Sasa Kabla sijapita na huu mlango mpaka ndani na kutibu jeuri yako nitapokubutua
Ngoja nahesabu moja mpaka tatu nauvunja maana nishagonga sana hadi vidole vimeungua
Majirani wananambia kuna njemba napishana nazo sana zinaingia mi nikiwa sipo
Na ndio maana unanambia nikitaka kuja niwe nakupigia leo nimetimba bila info
Hivi kitu gani nitakupa we mwanamke ukatulia
Ukatuliza na roho yangu ikatulia
Nshakuambia mara ngapi hujasikia
Na nazidi kurudia sasa leo utajutia nakuapia
Juzi juzi niliona tu umeshare snapchat uko level one na pembeni yako kuna mchizi
Nikadaka boda nikufate nafika sijakuona nikaambiwa kuwa ushasepa the deez
Najitahidi nisikuchunguze ila story zinanifikia na kiukweli zinanipa uchizi
Picha zako zote ndani ya gari tofauti unabadili tu mikao huku unachezea keys
Kuleta rafiki zako wa kiume kwenye nyumba niliyokupangia kwanza nshakupiga marufuku
Wanajiachia sebleni na vipensi wanacheza na rimoti kama wanachangia luku
Na hawatosheki na chakula unachowapikia maana wanakula mpaka yule anaewapikia
Navyogaramia na mateso unayonipatia hii nyumba mara mia nifugie kuku (kwenda)
Staki hizi mbichi ooh naah
Ukakasi mwingi staki staki staki hili bichi ooh naah
Kukupenda staki hii ni homa
Nimekoma tena staki staki hii sonona, noma
Kuna namba umeisave Daddy kwenye simu yako
Nimeshtuka hata kumbe huyo sio babaako
Unajifanya huna makuu bonge la pretender
Kuna story nimeskia sikuhizi we ni blender
Fungua, kabla sijasema vyote fasta fasta
Fungua, lazima nitapata kesi navunja kitasa
Fungua, staki ufala leo utapata unachokitaka
Fungua, mapenzi nikache staki, bomboclat!!!
Kabla sijakuacha nitakufunza adabu bwana utaempata huko atakuta umeshashika adabu
Hizi tabu juu ya tabu nimeshindwa ustaarabu
Kama Ndoa nishatoa kwenye hesabu ushanikata vibe
[Nkunda star]
Speaking venacular
Heee bhagosha
Sasa unamgongea nani sasa hapo wewe?
Una… yaa yani mi nimelala nasikia tu makelele unamgonga.. unagonga.. unamgongea nani sasa?
Hapo si nyumbani kwako wewe hapo?
Unalala na nani hapo? Humo sijawahi kuona hata umeleta ka demu mdomo wenyewe zege huo
Aisee hii mihadarati hii
Bora Serikali iendelee kukomesha hii mihadarati
Na iendelee kuzuiliwa hivi hivi kwanini sasa mtu unagonga mlango wako halafu unasema mtu akufungulie
Hebu ingia ndani ulale huko
Unatuchanganya watu tumelala bwana
Eee hii imeingia hii
Credits

About “Fungua” by Rapcha

Read the complete lyrics to "Fungua" by Rapcha from the album "To The Top Vol.2" in 2023. On Lyrks you can follow along with the full text, explore the artist's discography, and discover related songs. The track is often categorized under Rap.

"Fungua" is performed by Rapcha. from the album "To The Top Vol.2" in 2023 This page provides the full lyric text for fans who want to sing along, study the songwriting, or compare versions across releases. Lyrks organizes lyrics by artist and song slug so you can bookmark and share a stable URL. Music lyrics help listeners connect with emotion, narrative, and rhythm in a track. Whether you are learning English, researching a favorite chorus, or preparing for karaoke, having accurate line breaks and section labels (verse, chorus, bridge) makes the experience easier. We link to the official artist profile on Lyrks where available, including biography snippets, top songs, and chart placements when we have that data. If you enjoy "Fungua", explore more songs by Rapcha using the links below. Chart and trending pages on Lyrks highlight what listeners are searching for this week. For copyright or correction requests, see our DMCA and contact pages.

View all songs and biography for Rapcha · Trending lyrics · Billboard Hot 100

Frequently asked questions

"Fungua" is credited to Rapcha. Songwriting credits may include additional writers listed on the release; check the credits section on this page for linked collaborators.

"Fungua" appears on "To The Top Vol.2" in 2023.

Visit the Rapcha artist page at /artist/rapcha for biography, popular tracks, and links to more lyric pages.