Lyrks
Lyrks
Lyrks
Cover Art

Nyumbani ni Nyumbani Lyrics by TMK Wanaume Family

Ndio Zetu

0

[Instrumentals]
Sha! Sha!
[Verse 1: Mh Temba]
T.M.K (?)
Kwetu uswahilini, (Duh)
Huwezi kuamini wanaishi makachaa maskini
Home sweet home' bwana napazimia mimi
Kiwanja nikafate nini? (Eh)
Kwetu nyumbani, maharage bora kuliko nyama
Anayapikaga mama, mimi ndiyo nayapenda sana...
Hapa hapa ndio nyumbani
Mjomba Hassani (Eh)
Washa koroboi, humu ndani mbu wamezidi, wanakwenda jino kwa jino, wana uma mpaka kisigino
Sa ntalala wapi?
Mkataa kwao ni mtumwa, na akikua atakuwa mwanga
Kumbe anataka Lager; akilewa akabwage manyanga
Maji hayawashi gari, petroli haizimi moto, we mtoto
Ubishoo haufai!
Kwenu ni kwenu tu, hatakama hamnywi chai
Bu-bu-be!
Bu-bu-be!
Bu-bu-bu-bu- (Anhaa!)
[Verse 2: KR Mullah]
Nyumbani ni nyumbani' hatakama kichakani (Ndio)
Una act unakaa Upanga, kumbe mtoto wa Keko Mwanga
Na tena' kuna tetesi ya kuwa bibi yako mwanga (Sana...)
Uongo sio dawa, kwenu ni kwenu hatakama mko majalala, mmeuawa
Kwenu huonekani, wash'kaji wakija una wakaribisha kwa jirani (Ayaa...)
Tena ndo wa kwanza kushika remote control
Mwenye nyumba anakuchora, anakuona tu bishoo (Sana)
Ridhika na unachokipata, hivi ni kitu gani haswa kinacho kufanya hadi ukaazime pamba?
Nyumbani ni nyumbani, hatakama hujatoa kitu, hiyo sio kitu
Usibabaike na majina, usione wanakaa uzunguni, lakini sometimes ki-China (Ndiyo)
We mbongo akili zako mbona za kitoto?
Iwejе Sista Doo umnunulie chips, ukale mihogo?
Ma-Braza men kwa kutafuta sifa'
Wana shinda Masaki, wanalala Tandika (Noma...)
[Chorus: Juma Nature]
Shibе! Shibe! (Haina Bei!)
Shibe! Shibe! (Haina Bei!)
Shibe! Shibe! (Haina Bei!)
Shibe! Shibe! (Haina Bei!)
Hela ya kula nyumbani... (Hainogi!)
Utakosa burudani... (Hainogi!)
Kwani nyumbani ni nyumbani, hatakama kichakani (Hainogi!)
[Verse 3: Chege]
Nyumbani ni nyumbani, kwa jirani sio kwako
Jishughulishe, komaa kichwa, tafuta ngawira, upate midako (Uh -Huh)
Usipende sana cheusi uweke (Ah!)
Huyu jamaa ana makeke (Ah!)
Anajifanya nguna halipandi kisa chips
Wakati kwao kila siku nguna kwa ngisi
Mtume!
Amehama kwao eti kisa hakuna umeme
Na ameshindwa hata' kumtambulisha mke wake eti kisa ana figa ya kiume
Karibu, karibu, karibu nyumbani, jirani
Karibu pita mpaka barazani
Chagua moja, kujimwaga mkekani au jamvini?
[Verse 4: Mzimu]
Usidharau kwenu, (Eh)
Hiyo haifai, tena nishai
Au kwakuwa asubuhi hakupikwi chai? (Duh!)
Kwako ni kwako, si ndiyo chimbuko la wazazi wako? (Eh)
Hata kukiwa vipi, maji ya chumvi, gari haipiti
Ndo nyumbani hapo, we jivunie' ndo mungu alivyokupa' usichukie
Dagaa twende kazi, mambo nnayoeleza ndo kama dozi
Eehn...hiyo idea!
Ukila; kausha' sio unataja
Au kwakuwa umekua' palipo kulea una pateua (Haifai!)
Hii dunia bwana, isiwe ina kuzuzua
Nyumbani ni nyumbani, tia timu
Mzimu!
[Verse 5: Dollo]
Kwenu ni kwenu' hatakama kume ezekwa pamoja, sio hoja!
Siwezi kuwa laumu, najua sote ni wa moja
Mbona si ni wale wale, kila siku mlo mmoja
Maisha yetu ya dhiki, bado tuna vumilia dhiki (Wewe!)
Inakuwaje vipi mwenzetu utu tangazie dhiki?
Unakimbia bure nyumbani' unalala kwa marafiki,(Uh)
Unalala kwa majirani,(Uh)
Una zurura zurura tu, hujulikani tu mtoto wa nani (Mtoto wa nani)
Jutia nafsi yako, ujue nini unacho kifanya (Wewe!)
Wazazi una waeka wasiwasi, juu kiulizo alama (Hawana raha)
[Chorus: Juma Nature]
Shibe! Shibe! (Haina Bei!)
Shibe! Shibe! (Haina Bei!)
Shibe! Shibe! (Haina Bei!)
Shibe! Shibe! (Haina Bei!)
Hela ya kula nyumbani... (Hainogi!)
Utakosa burudani... (Hainogi!)
Kwani nyumbani ni nyumbani, hatakama kichakani (Hainogi!)
[Verse 6: Luteni Kalama]
Wanaume! (Eh!)
Tujitume! mtume... Aah!
Tusikate tamaa tu' tusonge mbele, tuwe makini
Jovir na twanga, na piga miamo ya chini
P-p-p Funk toleka!
Mwanaume hasifiwi sura, pilika na kuhangaika (Ihuu!)
Hii kitu kati' moto bati toka Nsoma mpaka Maruku
Wese haliendi tupu, nyumbani ni nyumbani hatakama patupu
Tia maguu nyumbani, udate!
Nyuma mpaka mbwa (Nyoo...)
Mtu akilala ndani, mwenzio' unamwona!
Isipo nyesha mvua ujue' siku hiyo tumepona!
Hapaeleweki eleweki, pako feki feki
Ndipo nilipozaliwa Kalama Bakari Salum (?)
Njengekemkeni (?) hadi wa mitomingi
Hapa ndipo pa dingi, nyumbani karibu mpaka ndani
Ni home maskani, nyumbani' panaitwa (?) komesa kwa Bi.Mkubwa...
Wanapoishi ma stelingi, ma dingi wa shua faza; na maza...(Yup)
(?)
Mbele kwa mbele, juu kwa juu (Aminia)
Wapo watu wenye ujiko; na roho za ki bitozi
Ukimuuliza hapa ndiyo nyumbani kwenu?
Anakataa, anataja kwingine, (Ma cheki Bobu)
Pale... kwenye nyumba ya vigae
Nje kuna Prado na Muso
Wakati tupo kwenye kituo, stori nyingi, Wassup nyingi
Anavunga' anazunguka na basi, ana vunga anakaa Masaki, kwenda kwao hataki
Kwenu, kwenu kukiwa mayebo kwenu
Kukiwa arosto kwenu
Ukienda kwao' uta mhurumia
Omba maji basi, Ah! friji mbovu msh'kaji
Niwekee movie, Ah! deki iko kwa fundi (Ayaah)
Katoa namba za simu feki, ukipiga' unaambiwa
"Samahani kaka umekosea namba huyu jamaa hakai hapa"
[Chorus repeat]

About “Nyumbani ni Nyumbani” by TMK Wanaume Family

Read the complete lyrics to "Nyumbani ni Nyumbani" by TMK Wanaume Family from the album "Ndio Zetu". On Lyrks you can follow along with the full text, explore the artist's discography, and discover related songs. The track is often categorized under Rap.

"Nyumbani ni Nyumbani" is performed by TMK Wanaume Family. from the album "Ndio Zetu" This page provides the full lyric text for fans who want to sing along, study the songwriting, or compare versions across releases. Lyrks organizes lyrics by artist and song slug so you can bookmark and share a stable URL. Music lyrics help listeners connect with emotion, narrative, and rhythm in a track. Whether you are learning English, researching a favorite chorus, or preparing for karaoke, having accurate line breaks and section labels (verse, chorus, bridge) makes the experience easier. We link to the official artist profile on Lyrks where available, including biography snippets, top songs, and chart placements when we have that data. If you enjoy "Nyumbani ni Nyumbani", explore more songs by TMK Wanaume Family using the links below. Chart and trending pages on Lyrks highlight what listeners are searching for this week. For copyright or correction requests, see our DMCA and contact pages.

View all songs and biography for TMK Wanaume Family · Trending lyrics · Billboard Hot 100

Frequently asked questions

"Nyumbani ni Nyumbani" is credited to TMK Wanaume Family. Songwriting credits may include additional writers listed on the release; check the credits section on this page for linked collaborators.

"Nyumbani ni Nyumbani" appears on "Ndio Zetu".

Visit the TMK Wanaume Family artist page at /artist/tmk-wanaume-family for biography, popular tracks, and links to more lyric pages.